Yanga imeaga michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa APR katika mchezo wa robo fainali
Jesus Moloko aliitanguliza Yanga mapema kwenye kipindi cha kwanza kabla ya APR kusawazisha katika dakika za lala salama kipindi cha kwanza
Kipindi cha pili Yanga ilipoteza umakini katika safu ya ulinzi na kujikuta wakiruhusu mashambulizi mengi kama APR wangeongeza umakini pengine wangepata ushindi mnono zaidi
Yanga imenufaika na michuano hiyo kocha Miguel Gamondi akiwapa nafasi nyota kutoka timu ya vijana pamoja na wachezaji ambao walikuwa hawatumiki zaidi katika kikosi cha kwanza
Wananchi wanarejea Dar kuendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi zijazo ligi kuu na ligi ya mabingwa
ADVERTISE HERE