Ni takribani siku sita zimesalia kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa Januari 15 2024, imefahamika Yanga inatarajiwa kufunga dirisha hilo na wachezaji wawili
Mpaka sasa Yanga imesajili wachezaji wawili katika dirisha hili ambao ni Shekhan Khamis na Augustine Okrah raia wa Ghana
Mabingwa hao wa soka Tanzania Bara pia wanahusishwa na kiungo mshambuliaji wa Union Maniema Basiala Agee
Eneo la safu ya ushambuliaji pia huenda likashuhudia maboresho katika siku chache zilizobaki kabla ya dirisha kufungwa
Hata hivyo ili kukamilisha usajili huo, Yanga itahitaji kuachana na nyota watatu wa kigeni
Uongozi wa Yanga uko kwenye mazungumzo na mshambuliaji Hafiz Konkoni ambaye tayari kocha Miguel Gamondi amemuondoka katika mipango yake
Imeelezwa kuwa Konkoni amegomea kutolewa kwa mkopo akitaka alipwe zaidi ya Tsh Milioni 300 kuvunja mkataba wake
Singida FG imeonesha nia kumtaka Jesus Moloko kwa mkopo huku beki Gift Fred nae akiwa kwenye hatihati