Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema wanakusudia kuhamisha ofisi na shughuli zote za klabu katika Jengo lililoko Makao Makuu ya klabu, Jangwani
Kumekuwa na ukarabati mkubwa unaoendelea katika jengo hilo ambapo Hersi amesema kufikia mwishoni mwa mwezi huu ukarabati huo utakuwa umekamilika
Akizungumza katika mahojiano maalum katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM jana, Hersi alisema maboresho hayo yatalifanya jengo hilo kuwa bora na la kisasa zaidi
"Tumefanya maboresho makubwa na ya kisasa kwenye jengo letu la Jangwani. Mungu akijalia mwishoni mwezi huu tutakuwa na jengo bora na la kisasa ambapo ofisi na shughuli zote za Klabu zitafanyika pale," alisema
Aidha Hersi aliweka bayana kuwa hatua za awali za ujenzi wa uwanja wa Yanga katika eneo la Kaunda zimeanza