Shekhan kufuata nyayo za Abdi Kassim?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jan 2024
Shekhan kufuata nyayo za Abdi Kassim?

Wachezaji kutoka visiwani Zanzibar wamekuwa na historia ya aina yake na klabu ya Yanga tangu zamani

Abdi Kassim 'Babi' ni miongoni mwa wachezaji waliojipatia heshima kubwa kipindi wanaitumikia Yanga

Babi aliitumikia Yanga kati ya mwaka 2007 na 2010 akicheza mechi 65 na kufunga jumla ya mabao 29

Wengi wanamkumbuka Babi kwa uwezo wake wa kupiga mashuti makali kupitia guu lake la kushoto

Mwaka 2017 Babi alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao uwanja wa Benjamin Mkapa katika siku ya ufunguzi kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania dhidi ya Uganda

Babi alipiga kombora akiwa karibu na mstari unaogawa uwanja na kombora hilo likaihesabia Tanzania bao pekee la mchezo huo

Hivi karibuni Yanga imemsajili kiungo kinda Shekhan Khamis kutoka klabu ya JKU ya Zanzibar

Shekhan anafananishwa na Babi kwa aina yake ya uchezaji na uwezo wake mkubwa wa kupiga mashuti

Akiwa na umri ya miaka 18 tu, Shekhan tayari ameanza kuwatisha walinda lango kutokana na makombora yanayotoka katika guu lake la kushoto

Katika mchezo wa robo fainali kombe la Mapinduzi ambao Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1, Shekhan alionyesha umahiri wake wa kuachia michomo mikali

Kama sio uhodari wa mlinda lango wa APR pengine angeweza kufunga bao kupitia moja ya mipira ya adhabu aliyopiga

Shekhan ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa bila shaka atadhihirisha umahiri wake katika kikosi cha kocha Miguel Gamondi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’