Kikosi cha Yanga kiliwasili mkoani Kagera mapema leo tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa kesho Ijumaa katika uwanja wa Kaitaba, saa 10 jioni
Yanga inatarajiwa kukamilisha maandalizi ya mwisho jioni ya leo katika uwanja wa Kaitaba
Katika kikosi yumo mshambuliaji mpya, Joseph Guede ambaye ni juzi tu alitambulishwa kuwa Mwananchi
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi huenda akamtumia Guede katika mchezo huo ambao Yanga inazihitaji alama zote tatu ili irudi kileleni mwa msimamo wa ligi
Guede amekuwa na takrbani siku tano za kujifua na wachezaji wenzake, ameonekana yuko tayari kushuka dimbani
Ni shauku ya mashabiki wa Yanga kumshuhudia nyota huyo mpya, bila shaka watamuona dimba la Kaitaba
ADVERTISE HERE