Baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Kagera Sugar, kikosi cha Yanga hakina muda wa kupoteza kwani kinarejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo unaofuata
Jumatatu, Februari 05 Yanga itashuka uwanja wa Azam Complex kuumana na Dodoma Jiji katika mchezo mwingine muhimu
Yanga inazihitaji alama zote tatu ili kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi, vijana wa Miguel Gamondi hakuna nafasi ya kurudia makosa ya mchezo uliopita
Kocha Gamondi amesema hawakucheza vizuri mchezo dhidi ya Kagera Sugar akiwataka wachezaji wake kujituma zaidi katika mchezo unaofuata
"Kusema ukweli hatukustahili kushinda mchezo dhidi ya Kagera Sugar kwa sababu hatukucheza kama mabingwa. Nakubali kulikuwa na matukio ya hovyo ya kupoteza muda kwa wapinzani wetu hasa kwenye dakika 15 za mwisho lakini kwa upande wetu hatukufanya zaidi," alisema Gamondi