Yanga imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu ya NBC baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji
Wananchi walilazimika kusubiri mpaka dakika ya 85 kushangilia bao lililowekwa kambani na Mudathir Yahya akimalizia pasi ya Nickson Kibabage
Sehemu kubwa ya mchezo huo ilitawaliwa na Yanga lakini kukosekana kwa umakini kulipelekea kupoteza nafasi nyingi hasa kwenye kipindi cha kwanza
Ni alama tatu muhimu kwa Yanga ambazo zimewarejesha kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 34
ADVERTISE HERE