Leo ni Birthday Yanga, mabingwa wa kihistoria wakitimiza miaka 89 tangu kuundwa mwaka 1935
Kilele cha maadhimisho hayo ni mkoani Mbeya kunako dimba la Sokoine katika mchezo wa ligi kuu Yanga wakiwa wageni wa Tanzania Prisons
Shamrashamra za maadhimisho haya zilianza jana kwa matukio mbalimbali katika jiji la Mbeya mashabiki na wanachama wa Yanga wakisafiri kutoka mikoa mbalimbali kwa ajili ya siku hii
Hii ni siku ya Wananchi na haitapendeza kama Yanga itakosa ushindi katika mchezo dhidi ya Prisons
Kikosi cha Yanga kilitua Mbeya jana jioni tayari kwa mchezo huo utakaopigwa saa 10 jioni
Kinara wa mabao ligi kuu ya NBC Stephane Aziz Ki ni sehemu ya waliosafiri mkoani Mbeya na pengine leo atarejea kuendeleza pale alipoishia kabla ya kwenda kwenye michuano ya Afcon 2023 inayofikia tamati leo kwa mchezo wa fainali kati ya Ivory Coast dhidi ya Nigeria