Mudathir ukimuona tu, jua kazi ipo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Feb 2024
Mudathir ukimuona tu, jua kazi ipo

Mudathir Yahya ni mchezaji ambaye pengine hazungumzwi sana kama ilivyo kwa nyota wengine wa Yanga kama Stephane Aziz Ki, Pacome na hata Maxi Nzengeli

Lakini Mudathir ni mmoja wa wachezaji muhimu katika kikosi cha Yanga, ameendelea kuthibitisha hilo uwanjani

Ni mchezaji anayeweza kutumika kimkakati zaidi, alimtumia hivyo Nasreddine Nabi na hata Miguel Gamondi amekuwa akimtumia hivyo

Katika ligi kuu ya NBC msimu huu, Mudathir amepachika mabao manne, mabao yake matatu yalichangia alama tisa za Yanga. Ni katika zile mechi ambazo Wananchi walikuwa wamepoteza matumaini ya ushindi

Alifunga bao la ushindi katika mchezo dhidi ya Namungo Fc (dkk 85), akafunga dhidi ya Dodoma Jiji (dkk 86) na pia dhidi ya Mashujaa Fc (dkk 86) lakini pia alifunga bao dhidi ya KMC katik ushindi wa mabao 5-0

Mudathir pia ana bao moja kwenye michuano ya ligi ya mabingwa akifunga katika mchezo dhidi ya Medeama uliopigwa jijini Dar es saalaam Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0

Mudathir ameeleza siri ya mafanikio yake ni kufuata maelekezo anayopewa na Walimu wake katika kiwanja cha mazoezi

Tangu ujio wa Gamondi Mudathir amejihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza akianza eneo la kiungo sambamba na Khalid Aucho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’