Katika misimu iliyopita unaweza kusema Yanga ilikuwa ikitabirika, ilikuwa rahisi kwa makocha wa timu pinzani kufahamu wamdhibiti nani katika mechi dhidi ya Yanga
Katika misimu miwili iliyopita, mshambuliaji Fiston Mayele ndiye aliyekuwa akibeba ramani ya vita ya Yanga
Mayele ndiye aliyekuwa akifunga mabao mengi na pale alipokosekana mambo yalikuwa magumu kwa Kocha Nasreddine Nabi
Lakini tangu ujio wa Miguel Gamondi mambo yamebadilika, kikosi chake hakitabiriki
Wachezaji wanaocheza eneo la kiungo ndio wanafunga mabao zaidi kuliko safu ya ushambuliaji
Kwenye ligi msimu huu Yanga imefunga mabao 39, mabao 30 yamefungwa na viungo. Washambuliaji na mabeki wakafunga mabao mengine 9
Stephane Aziz Ki ana mabao 10, Maxi Nzengeli ana mabao 8, Pacome Zouzoua na Mudathir Yahya kila mmoja ana mabao 6
Ukiangalia mechi nne zilizopita, Mudathir amepachika mabao manne huku Pacome akifunga mabao mawili, Maxi bao moja na Mzize bao 1
Yanga hii ambayo inalalamikiwa ina changamoto kwenye safu ya ushambuliaji inafunga sana kuliko wakati mwingine wowote
Gamondi amefanikiwa kuifanya Yanga isiwe tegemezi kwa mchezaji mmoja