Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewataka wapenzi na wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Azam Complex kesho Jumanne katika mchezo wa kombe la FA raundi ya tatu dhidi ya Polisi Tanzania
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Kamwe amesema benchi la ufundi limependekeza waendelee kucheza mechi zao kama ratiba inavyoelekeza ili kuwaweka wachezaji katika hali ya ushindani kuelekea mchezo dhidi ya CR Belouizdad
"Kuna tofauti kubwa kati ya mazoezi na mechi. Kwa kuzingatia mapendekezo ya benchi letu la ufundi sisi tumekubaliana tutacheza mechi zetu kama ratiba ilivyoelekeza"
"Hatuna haja ya 'kudeka deka' hivyo mashabiki mje kwa wingi uwanja wa Azam Complex kesho Jumanne katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Polisi Tanzania"
"Tutaitumia mechi hii kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya CR Belouizdad"
"Viingilio vya mchezo huo VIP A ni Tsh 20,000/-, VIP B Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-"
"Sisi hatuna mambo ya kulazalaza mechi, hakuna mambo ya kuweka viporo hapa," alisema Kamwe