Kabla ya kuikabili CR Belouizdad pale uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi leo Yanga itakuwa uwanja wa Azam Complex kuikabili Polisi Tanzania katika mchezo wa raundi ya tatu kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amegoma vijana wake kukaa muda mrefu pasipo kucheza mechi kwani jambo hilo linaweza kuathiri utimamu wao katika mechi muhimu inayofuata ligi ya mabingwa dhidi ya CR Belouizdad
Yanga itatumia mchezo dhidi ya Polisi Tanzania kama sehemu ya maandalizi ya kumkabili Mwarabu Jumamosi
Bila shaka Gamondi leo atafanya 'rotation' ya kikosi chake, nyota ambao hawakutumika katika mechi iliyopita ya ligi kuu dhidi ya KMC huenda wakapata nafasi ya kuanza leo
Kabla ya kuelekea Azam Complex, kuanzia asubuhi Wananchi watakuwa Mbagala Zakhiem katika hamasa ya kuelekea mchezo dhidi ya Belouizdad