Kama mshambuliaji Joseph Guede angekuwa makini basi jana angeondoka na mpira 'hat-trik' katika mchezo wa raundi ya tatu kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Polisi Tanzania
Guede alipachika mabao mawili katika mchezo huo yote yakitokea mguuni kwa winga Augustine Okrah ambaye alitengeneza nafasi nne za wazi, mbili zikitumika Guede akikosa moja ya nafasi adimu katika ushindi wa mabao 5-0
Kasi ya Okrah ilikuwa tatizo kwa walinzi wa pembeni wa Polisi Tanzania, lakini pia krosi zake zilirahisisha kazi ya Guede katika umaliziaji
Gamondi amefurahia kazi iliyofanywa na Okrah jana, akiamini ameongeza mtu mwingine ambaye ataongeza ufanisi eneo la ushambuliaji
Lakini pia Okrah ni kama amewatumia salamu kina Maxi Nzengeli, Pacome na hata Aziz Ki kuwa anataka nafasi katika kikosi cha kwanza
Ni bahati mbaya alichelewa kuanza majukumu yake Yanga baada ya kuumia kwenye michuano ya kombe la Mapenduzi
Ni majeraha hayo aliyopata kwenye 'mgomba wa pua' yanamfanya avae 'mask' ili kuepuka madhara zaidi
Aina ya majeraha aliyopata yanaweza kuchukua hadi miezi minne kupona kabisa