Yanga, Karimjee Mobility zaingia makubaliano

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Feb 2024
Yanga, Karimjee Mobility zaingia makubaliano

Klabu ya Yanga na Karimjee Mobility leo wamesaini Mkataba wa ushirikiano wa miezi 18 ambao utaishuhudia Yanga ikivuna Tsh Milioni 300

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema Karimjee Mobility kupitia kampuni ya Hero wanatengeneza na kusambaza pikipiki katika Mataifa zaidi ya 40

Kupitia makubaliano hayo, Yanga na Hero watakuwa washiriki wa kibiashara katika muda wote wa mkataba

"Leo tumeingia makubaliano na kampuni ya Karimjee Mobility kupitia kampuni ya Hero ambayo inatengeneza pikipiki na kusambaza. Kampuni ya Hero inatajwa kuwa kampuni namba 1 duniani kwa biashara hiyo. Kampuni hii kutoka India inafanya biashara mataifa zaidi ya 40. Young Africans SC itapata kiasi cha Tsh Milioni 300 kutoka kwenye mkataba huu katika kipindi cha miezi 18"

"Mkataba huu utaruhusu kwa matawi yetu ya Klabu kupata posho kwenye mauzo ya pikipiki hizo. Kwahiyo kila tawi linapaswa kuhakikisha biashara hii inakuwa kwa kasi. Hivyo basi kila mwananchi pikipiki yako ya kununua ni Hero na pikipiki ya kutumia ni Hero"

"Tuwahakikishie kampuni ya Hero kuwa sisi ni Klabu namba moja na tutahakikisha @heromototanzania ambao ni namba moja waendelee kubakia kuwa namba moja. Uwezo wa kuifanya Hero kuwa namba moja ni jukumu la kila Mwanachama wa Young Africans, hivyo kuanzia sasa bodaboda ni Hero," alisema Hersi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’