Baada ya kujihakikishia tiketi ya kucheza robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Wananchi bado hawajamaliza kwani malengo sasa ni kusaka ushindi nchini Misri na kumaliza vinara wa kundi D
Kikosi cha Yanga leo kimerejea mazoezini Avic Town kwa ajili ya maandalizi kabla ya safari ya Misri kwenda kuikabili Al Ahly
Ijumaa ya wiki hii, Yanga itaumana na Al Ahly katika mchezo ambao utaamua timu itakayomaliza nafasi ya kwanza kundi D
Mpaka sasa Al Ahly wako kileleni wakiwa na alama 9 Yanga ikiwa nafasi ya pili ikikusanya alama 8
Ni mchezo mwingine wa kuidhihirishia Afrika kuwa Yanga sasa iko tayari kushindana na yeyote iwe nyumbani au ugenini
ADVERTISE HERE