Leo ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki
Msimu wake wa pili na Yanga umekuwa bora sana akiwa mmoja wa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kocha Miguel Gamondi
Baada ya kushiriki kikamilifu kuipeleka Yanga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Aziz Ki anarejesha makali yake kwenye ligi akiisaka tuzo ya ufungaji bora msimu huu
Mabao yake 10 yanamfanya kuwa kwenye nafasi nzuri katika kinyang'anyiro licha ya kuzidiwa bao moja na Feisal Salum wa Azam Fc
Azam Fc imecheza mechi tatu zaidi ya Yanga hivyo Aziz Ki anayo nafasi ya kufunga zaidi ya bao 1 katika mechi hizo
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake
HAPPY BIRTHDAY AZIZ KI...!
ADVERTISE HERE