Tuko tayari kucheza na yeyote robo fainali - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Mar 2024
Tuko tayari kucheza na yeyote robo fainali - Kamwe

Meneja wa habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema Yanga iko tayari kucheza na yeyote katika hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Yanga ni miongoni mwa timu nane zilizotinga robo fainali ambapo droo ya hatua hiyo itafanyika Jumanne ijayo nchini Misri

Kulingana na mpangilio wa CAF, Yanga itapangwa dhidi ya timu iliyoongoza kundi A,B au C ambazo ni Mamelodi Sundowns, Asec Mimosas au Petro Atletico

Kamwe amesema timu zote ni bora ndio maana ziliongoza makundi hivyo watakuwa tayari kucheza na yeyote

"Katika hatua ya robo fainali sisi hatumuhofii yeyote. Tunatambua timu zote ambazo tuna nafasi ya kupangwa nazo ni nzuri ndio maana ziliongoza makundi yao"

"Kama ingekuwa ukiingia robo fainali unaruhusiwa kuchagua mpinzani wako basi yupo ambaye tungemchagua ili tumalize utata mapema"

"Lakini kwa utaratibu ulivyo, basi tunaisubiri droo hiyo tufahamu tutachuana na nani lakini kimsingi tutakuwa tayari kucheza na yeyote," alisema Kamwe

Katika timu zilizotinga robo fainali, Mamelodi Sundowns inaonekana kuhofiwa zaidi kutokana na ubora walioonyesha katika michuano ya msimu huu

Sundowns ndio, mabingwa wa AFL, michuano iliyofanyika Afrika kwa mara ya kwanza mwaka huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
34m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’