Gamondi ataja sababu baadhi ya wachezaji kubaki Dar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Mar 2024
Gamondi ataja sababu baadhi ya wachezaji kubaki Dar

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema baadhi ya wachezaji hawatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Namungo Fc leo katika mchezo wa ligi kuu ya NBC kutokana na sababu mbalimbali

Wachezaji Djigui Diarra, Khalid Aucho, Joyce Lomalisa, Pacome Zouzoua, Kennedy Musonda na Joseph Guede hawakuonekana katika mazoezi ya mwisho yaliyofanyika dimba la Majaliwa jana jioni

Gamondi amesema kila mchezaji aliyebaki ana sababu ya msingi ambapo wapo wenye majeraha na wengine kuwa na matatizo ya kifamilia

"Kwa asilimia kubwa ni wachezaji muhimu kikosini, lakini wana shida ambazo tungeziweka pembeni ingeleta shida kwani wasingecheza kwa ubora tunaoufahamu kutoka kwao"

"Sipendi kuweka wazi shida ya kila mmoja inatakiwa kueleweka kuwa kuna ambao wana majeraha madodo madogo na wengine shida za kifamilia," alisema

Gamondi aliongeza kuwa nyota hao wataweza kurejea katika mechi zinazofuta ambapo baada ya mechi ya leo Yanga itacheza mechi nyingine tatu dhidi ya Ihefu Fc, Geita Gold na Azam FC

"Baada ya mechi ya leo na Namungo tutakuwa na siku mbili tu tayari kwa mchezo mwingine wa ligi, hivyo kutoa nafasi za baadhi ya wachezaji ambao hawapo fiti kutokana na majeraha madogo madogo itatusaidia," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
16m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’