Yanga, Simba uso kwa uso Ligi ya Muungano

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Mar 2024
Yanga, Simba uso kwa uso Ligi ya Muungano

Miaka ya nyuma kulikuwa ligi ya Muungano ambayo ilikutanisha timu za Tanzania Bara na Zanzibar, michuano hiyo inatarajiwa kurejea mwaka huu

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF), Hussein Ahmada Vuai, amesema kwa kuanzia watakuwa na timu nne, mbili kutoka Tanzania Bara na mbili kutoka Zanzibar

Klabu za Yanga na Simba zitaiwakilisha Tanzania bara na upande wa Zanzibar ni KMKM na KVZ. Upo uwezekano mkubwa wa derby ya Kariakoo kushuhudiwa visiwani Zanzibar

"Ni kweli Kombe la Muungano limerejea na kuanzia tutaanza na klabu nne, mbili kutoka Tanzania Bara na mbili kutoka visiwani Zanzibar,’’ alisema Vuai.

Vuai alizitaka klabu hizo kuwa ni Simba na Yanga kwa Tanzania Bara na KMKM na KVZ kwa upande wa Zanzibar. Hata hivyo, amesema kuwa kwa msimu huu wameanza na timu hizo, lakini mwakani wanatarajia kuongeza timu na kufikia nane, ambapo kila upande utatoa timu nne

"Mara hii tumeanza na timu hizo kutokana na ratiba kuwabana kwa kila upande ambapo wenzetu kutoka Tanzania Bara wanakabiliwa na mashindano ya kimataifa pamoja na kuwapo kwa AFCON kuliathiri ratiba za ligi na kuwa na viporo vingi"

Vigezo ambavyo wamevitumia katika kuzipata timu hizo ni kuchukuwa mshindi wa kwanza na wa pili wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara na Visiwani na kwamba ratiba kamili itatolewa ili kujua nani atacheza nani ikiwa ni pamoja na kutangaza zawadi na mdhamini ambaye atadhamini michuano hiyo

Hata hivyo, amesema timu hizo zitacheza kwa mtindo wa mtoano na fainali itachezwa siku ya kilele cha sherehe za Muungano Aprili 26, mwaka huu. 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’