Katika benchi la ufundi la Yanga, yupo Mpho Maruping raia wa Afrika Kusini. Huyu ndio mtaalam wa kusoma mbinu za wapinzani kupitia video (Video Analyst)
Kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika kati ya Yanga dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa March 30, Maruping amepewa jukumu la kumrahisishia kazi kocha Miguel Gamondi
Mpho anaifahamu vyema Mamelodi, akicheza mechi nyingi za ligi kuu ya Afrika Kusini lakini pia akifanya majukumu yake katika timu ya Taifa
Uwepo wake benchi la ufundi la Yanga, ni kuwa silaha muhimu sana kwa Wananchi kuelekea mchezo dhidi ya Mamelodi
Yanga na Mamelodi zinafanana katika aina ya soka wanalocheza, kitakachowatofautisha ni maandalizi ya kimbinu na timu ipi itatumia vyema makosa ya mpinzani wake
Mpaka sasa Gamondi tayari ana taarifa za kutosha kuhusu Mamelodi, kilichobaki ni kuandaa mbinu sahihi za kuwamaliza pale kwa Mkapa March 30