Waliokuwa timu za Taifa kurejea Jumatano

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Mar 2024
Waliokuwa timu za Taifa kurejea Jumatano

Wachezaji wote wa Yanga waliokuwa katika majukumu ya timu za Taifa wametakiwa kuripoti kambini Avic Town siku ya Jumatano kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema kocha Miguel Gamondi amehitaji angalau siku mbili za maaandalizi ya mwisho akiwa na wachezaji woteΒ 

"Wachezaji wote ambao wako katika majukumu ya timu za Taifa wanatakiwa kurejea nchini Jumatano, March 27. Mwalimu Gamondi anahitaji angalau siku mbili za maandalizi ya mwisho akiwa na wachezaji wote"

"Hivyo matarajio yetu ni kuwa wote watarejea Jumatano hata kama itakuwa usiku wa manane, watahitajika kuripoti Avic Town," alisema Kamwe

Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto na Aboutwalib Mshery ambao walibaki Azerbaijan na timu ya Taifa ya Tanzania, walimaliza majukumu yao jana na wanatarajiwa kurejea nchini leo wakiwa na kikosi cha Stars

Kennedy Musonda, Pacome Zouzoua, Djigui Diarra na Stephane Aziz Ki timu zao za Taifa zikishuka dimbani leo kukamilisha ratiba za mechi za kirafiki

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’