Wachezaji wa Yanga wako tayari kwa mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa Jumamosi March 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amefichua kuwa wachezaji wanafanya mazoezi kwa ari kubwa kwa ajili ya mchezo huo dhamira ikiwa kushinda na kuwapa furaha Wananchi siku ya Jumamosi
Kamwe amesema wachezaji wanafuatilia mijadala katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, wameona ni kwa kiasi gani hawapewi nafasi ya kufanya vizuri dhidi ya Mamelodi, hii imekuwa chachu kwao kujituma zaidi
"Jana usiku saa 5 alinipigia simu Mudathir, akiwa anafanya mazoezi binafsi. Wachezaji wote walikamilisha mazoezi saa 12 lakini Muda alirejea tena uwanjani kujifua saa 5"
"Katika moja ya mamba tuliyozungumza aliniambia ni kwa kiasi gani wachezaji wanaitaka mechi dhidi ya Mamelodi ili kudhihirisha ubora wao tofauti na vile ambavyo baadhi ya wachambuzi wanawachukulia"
"Mudathir amenihakikishia katika mchezo huu Wananchi watarajie kuiona Yanga tofauti kabisa kuliko wakati mwingine wowote," alisema Kamwe
Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi dimba la Mkapa siku ya Jumamosi kwani itakuwa siku ya furaha kubwa kwao