Kambi ya Yanga imenoga baada ya nyota waliokuwa timu za taifa kurejea na moja kwa moja kuungana na wenzao kujiandaa na mechi ta robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns itakayopigwa Jumamosi March 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga ilikuwa na wachezaji 9 waliokuwa katika majukumu ya timu za Taifa, wote wamerejea wakiwa fit kuelekea mtanange huo wa kuamua timu itakayofuzu nusu fainali
Pacome Zouzoua, Diarra Djigui, Stephane Aziz KI, Kennedy Musonda, Aboutwalib Mshery na Bakari Mwamnyeto walichelewa kukamilisha majukumu yao ya timu za Taifa ambapo Pacome, Mwamnyeto, Musonda na Mshery walirejea juzi huku Diarra na Aziz Ki walitarajiwa kurejea usiku wa kuamkia leo
Yanga itavaana na Mamelodi kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 3:00 usiku kabla ya kwenda kurudiana wiki ijayo jijini Pretoria, Afrika Kusini na mshindi wa jumla atasonga nusu fainali kucheza ama na Esprance ya Tunisia au Asec Mimosas ya Ivory Coast.
Aidha kuhusu majruhi Kibwana Shomari, Khalid Aucho, Zawadi Mauya walishiriki mazoezi jana wakati Yao akiendelea kuwa chini ya usimamizi wa kocha wa viungo, Yossouf Ammar ili kuona kama anaiwahi mechi hiyo ya kesho