Kiungo Zawadi Mauya amesema wachezaji wako tayari kwa mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mauya amesema ari na morali ya timu iko juu dhamira yao ikiwa kushinda mchezo dhidi ya Mamelodi
"Sisi tuko tayari, tumekuwa na maandalizi mazuri kutoka kwa makocha wetu leo tutakamilisha maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Mamelodi"
"Mchezo huu una umuhimu wa kipekee kwetu kwani tunaona tunayo nafasi kufanya vizuri zaidi ya vile tulivyofanya kwenye kombe la Shirikisho msimu uliopita"
"Hii ni motisha kubwa kwani kama tukiweza kuvuka katika hatua hii tutatengeneza historia kubwa zaidi," alisema Mauya
Mauya ameongeza kuwa uzoefu waliopata katika kombe la Shirikisho msimu uliopita ni chachu kubwa kwao kufanya vizuri katika ligi ya mabingwa msimu huu