Aziz Ki amepania nusu fainali CAF CL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Apr 2024
Aziz Ki amepania nusu fainali CAF CL

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amesema wamejipanga kupata matokeo ambayo yatawahakikishia kutinga nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika katika mchezo wa pili wa robo fainali dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa huko Pretoria hapo kesho

Baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Dar es salaam wiki iliyopita, ushindi au sare yoyote ya mabao itaihakikishia Yanga kuvuka nusu fainali

Aziz Ki amesema mechi ya kwanza imewasaidia kuwafahamu vyema Mamelodi na sasa wanakwenda kupambana kupata ushindi katika mchezo huo wa pili

"Mechi itakuwa ngumu lakini Yanga tuna nafasi ya kufanya vizuri na kama tutapata matokeo basi yawe ya mapema kuwafanya wapinzani wawe na presha kubwa kutokana na matokeo ya mchezo uliopita"

"Kurejea kwa wenzetu waliokuwa majeruhi ni faida kwa kikosi chetu na tutahakikisha tunawafurahisha mashabiki waliosafiri na wale ambao tumewakuta Afrika Kusini"

"Hatuna presha tutacheza na Mamelodi tukiwa na malengo ya kutaka kufuzu, tumeshacheza nao tunawajua, tulipokuwa nyumbani tulifanya makosa ya kutotumia nafasi lakini ugenini tutafatuta bao au mabao ili kuwaweka kwenye presha wapinzani wetu," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’