Tuko tayari - Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Apr 2024
Tuko tayari - Gamondi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema timu iko tayari kwa mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaopigwa uwanja wa Loftus kesho Ijumaa

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Gamondi alisema kila timu ina nafasi sawa ya kutinga hatua ya nusu fainali

Amesema wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu lakini hawako Afrika Kusini kutembea, watapambana kuwania matokeo ya kuwapeleka nusu fainali

"Utakuwa mchezo mgumu lakini ni lazima baada ya dakika 90 kuwe na mshindi mmoja. Mpaka sasa mchezo uko 50/50 bado kila timu ina nafasi hivyo tuko hapa kuhakikisha tunapambana kupata matokeo mazuri," alisema Gamondi

Aidha kocha huyo raia wa Argentina amesema hawatishwi na historia ya Mamelodi Sundowns kwani anakiamini kikosi chake kina wachezaji wazoefu na wapambanaji

"Siwaandai wachezaji wangu kwa ajili ya historia ya Mamelodi, naandaa timu yangu kutokana na dakika 90 zinazokuja. Tunaamini kazi tuliyofanya kwenye Uwanja wa mazoezi, tuna imani na wachezaji na Mashabiki wetu, haitakuwa rahisi kwetu na kwao pia"

"Tuna Wachezaji wenye uzoefu wenye sifa ya kupambana, msimu uliopita kwenye Fainali ya Kombe la Shirikisho walipoteza nyumbani lakini wote mnajua kilichotokea walipokwenda ugenini, kesho ni mchezo tofauti lakini watapambana tena kwa ajili ya mashabiki wetu"

Akizungumzia hali za wachezaji waliokuwa majeruhi, Gamondi alisema kuna nafasi ya baadhi yao kurejea lakini hatma yao itafahamika baada ya mazoezi ya mwisho leo

"Tunasubiri kuona itakavyokuwa leo kwenye mazoezi ya mwisho, tunaweza kumpata mchezaji katika wale waliokuwa majeruhi. Ni kweli tunaiwaza nusu fainali ya CAF lakini tunajali pia na usalama wa afya za wachezaji wetu pia. Young Africans haichezi mashindano haya peke yake"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’