Yanga leo inatupa kete muhimu katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwa kuumana na Mamelodi Sundowns katika mchezo wa mkondo wa pili robo fainali
Mchezo huo utakaopigwa uwanja wa Loftus, utaunguruma kuanzia saa 3 tatu usiku
Ni mchezo wa kuamua hatma ya Yanga kucheza nusu fainali ya ligi ya mabingwa mwaka huu
Ushindi au sare yoyote ya mabao itaihakikishia Yanga kutinga nusu fanali na hivyo kutimiza malengo yake
Itakuwa kivumbi na jasho katika dimba la Loftus kwani Wananchi wamepania kuwaduwaza Sundowns katika uwanja wao wa nyumbani
Yanga inatarajiwa kupata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wake waliosafiri kutoka jijini Dar es salaam na wale ambao ni wakazi wa hapo Afrika Kusini
Msimu uliopita Yanga ilipokwenda kucheza na Marumo Gallants hapo Afrika Kusini, Wananchi walikuwa kama wako nyumbani kwani walikuwa na mashabiki wengi kuliko wenyeji wao
NI mechi ngumu lakini ni mechi ambayo Yanga imejiandaa kucheza. Zitakuwa dakika 90 za kivumbi na jasho katika uwanja wa Loftus