Leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga, Ali Kamwe
Baada ya Haji Manara kufungiwa na Hassan Bumbuli kuondoka Wananchi walipata wasi wasi juu ya uteuzi wa Kamwe kama angeweza kuitendea haki nafasi hiyo
Lakini mpaka sasa Kamwe amefanya mambo makubwa ambayo pengine hayakuwahi kufanywa na watangulizi wake
Leo hii Kitengo cha Habari na Mawasiliano ni miongoni mwa vitengo vinavyoingiza mapato mengi kwa Yanga
Yanga imetawala kila mahali, Kamwe na kitengo cha Habari wamefanya kazi kubwa na sasa Yanga ndio timu inayofuatiliwa zaidi katika mitandao ya kijamii hapa Tanzania na upande wa Afrika ikichuana na Al Ahly
Bila shaka siku hii itakuwa nzuri zaidi kwake pale Yanga itakapoibuka na ushindi dhidi ya Mamelodi Sundowns na kutinga nusu fainali CAF CL
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii muhimu kwake
HAPPY BIRTHDAY ALI KAMWE...!