Yanga kuongeza umakini mechi dhidi ya Dodoma Jiji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Apr 2024
Yanga kuongeza umakini mechi dhidi ya Dodoma Jiji

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, amesema watakuwa makini katika mchezo wa hatua ya 16-bora wa Kombe la CRBD Bank dhidi ya Dodoma Jiji FC, kwani ni timu iliyowasumbua kwenye mechi ya Ligi Kuu,

Kikosi cha Yanga kilitua mkoani Dodoma jana majira ya jioni na leo wanatarajiwa kufanya mazoezi yao ya mwisho katika uwanja wa Jamhuri utakaotumika hapo kesho

Gamondi amesema wamejipanga vizuri kulingana na mchezo huo kuwa mgumu kwani mashindano hayo ni mtoano na anayefungwa anatoka

Alisema walipata muda mfupi wa kufanya mazoezi kwa sababu ya kutoka katika mashindano makubwa na anatambua Dodoma Jiji FC mara ya mwisho iliwasumbua

"Haitakuwa mechi rahisi kwa sababu Dodoma Jiji FC ni wazuri na tuliwahi kucheza nao nyumbani na walitusumbua, mchezo huu tunatakiwa kuwa makini na kucheza kwa tahadhari kubwa ili kufuzu kucheza robo fainali," alisema Gamondi

Aliongeza kuwa wanahitaji kutetea mataji yao yote msimu huu na ili kufanikisha malengo yao ni kushinda mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji FC na kwenda kucheza robo fainali na baadaye nusu na kisha fainali

Gamondi amesema licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji kutokana na sababu mbalimbali, lakini anaimani na wachezaji waliopo fiti kwa mchezo huo kwenda kupambana na kupata matokeo mazuri

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’