Matchday : Dodoma Jiji vs Yanga, FA Cup

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Apr 2024
Matchday : Dodoma Jiji vs Yanga, FA Cup

Yanga leo itanogesha shamrashamra za sikukuuu ya Eid uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma itakapochuana na Dodoma Jiji katika mchezo wa kuwania tiketi ya kutinga robo fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB

Baada ya watani zao Simba kudondokea pua mbele ya Mashujaa Fc kwa kuondoshwa katika michuano hiyo jana, ni wazi Yanga leo itaingia katika mchezo huo ikiwa na tahadhari kubwa

Katika mchezo huo Yanga itawakosa nyota wake watatu Pacome Zouzoua, Yao Kouassi na Kennedy Musonda

Hata hivyo ni Musonda pekee ambaye alitumika katika mechi mbili za ligi ya mabingwa dhidi ya Memelodi Sundowns na leo kukosekana

Dodoma Jiji haijawahi kuwa timu nyepesi kila inapokutana na Yanga

Mara ya mwisho timu hizo zilikutana uwanja wa Azam Complex katika mchezo wa ligi kuu na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 Mudathir Yahya akifunga dakik ya 88

Mchezo huo utapigwa kuanzia saa 2 usiku..!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’