Aziz Ki aandaliwa mkataba mpya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Apr 2024
Aziz Ki aandaliwa mkataba mpya Yanga

Klabu ya Yanga imeanza mazungumzo ya kumuongeza mkataba kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu

Aziz Ki amekuwa na kiwango bora msimu huu akiwa kinara wa mabao katika ligi kuu ya NBC akifunga mabao 13 na kutoa pasi saba za mabao

Ni wazi ubora huo umezivutia timu nyingi ikiwemo klabu ya Mamelodi Sundowns ambayo inatajwa kuanza juhudi za chinichini kumshawishi nyota huyo raia wa Burkina Faso akajiunge nao

Ni baada ya kuwasumbua katika mechi mbili za robo fainali ligi ya mabingwa ambapo kocha wa Sundowns Rulani Mokwena alionekana kuvutiwa na uwezo wake. Mokwena alionekana kufanya mazungumzo na Aziz Ki baada ya mechi zote mbili

Hata hivyo Yanga iko katika nafasi nzuri ya kumbakisha kwa kuwa Aziz Ki mwenyewe anafurahia maisha yake na mabingwa hao wa Tanzania Bara

Aziz Ki ameweka wazi kuwa bado hajamaliza kazi iliyomleta Yanga hivyo hafikirii kuondoka kwa sasa na hakuna thamani yoyote ya pesa inayoweza kumshawishi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’