Baada ya kuichapa Wolaitta Dicha mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wa mtoano kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho Barani Afrika, morali ya ushindi kwenye kikosi cha Yanga imerejea.
Inaelezwa matokeo ya kutolewa na Singida United hatua ya robo fainali kombe la FA yaliwaumiza sana wachezaji hadi kuhofia pengine wasingefanya vizuri kwenye mchezo dhidi ya Dicha.
Inaelezwa kuwa baada ya mchezo ule mkoani Singida, benchi la ufundi ilibidi lifanye kazi ya ziada kuwatuliza kwani walipata huzuni kubwa.
Lakini ushindi dhidi ya Dicha umeweka matumaini ya kutinga makundi na jambo hilo limerejesha na kuinua morali ya wachezaji.
Keshokutwa April 11 Yanga inashuka uwanja wa Taifa kuikabili Singida United katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 22.
Katika mchezo huo huenda tukaishuhudia Yanga halisi ya Kimataifa kwani wachezaji wote wako tayari na wameiva hasa.
Matokeo ya ushindi ni muhimu ili kuendelea kuipa wakati mgumu Simba ambayo itacheza michezo zaidi wakati Yanga ikitekeleza majukumu ya Kimataifa

ADVERTISE HERE