Mawindo ya Simba kuanza Jumanne

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Apr 2024
Mawindo ya Simba kuanza Jumanne

Baada ya mapumziko ya siku moja, kesho Jumanne kikosi cha Yanga kitaanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi, April 20 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Yanga ilirejea jijini Dar es salaam mapema leo wakitokea Mwanza ambako jana waliichapa Singida FG mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alisema Kocha Miguel Gamondi amewapa wachezaji mapumziko ya siku moja na kesho watarejea Avic Town kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Simba

"Baada ya kurejea kutoka Mwanza, wachezaji wamepewa mapumziko ya siku moja na kesho Jumanne tutaanza maandalizi yetu ya mchezo wa dabi dhidi ya Simba"

"Tunauchukulia mchezo huu kwa umuhimu mkubwa kwani tunafahamu matokeo ya ushinda yatatuweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutetea ubingwa wetu kwa msimu wa tatu mfululizo," alisema Kamwe

Aidha Kamwe alibainisha kuwa wachezaji waliokuwa majeruhi kwa kiasi kikubwa wameimarika na tayari kurejea uwanjani

"Tumewona Khalid Aucho, Kibwana Shomari na Zawadi Mauya wakiwa wamerejea uwanjani. Lakini pia Yao Kouassi nae amepona wakati Pacome Zouzoua yuko katika awamu ya mwisho ya recovery yake"

"Musonda alipata majeraha madogo katika mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns, nae alipewa mapumziko na tunaamini nae atakuwa tayari kurejea uwanjani"

"Jambo muhimu tunakwenda katika maandalizi yetu kuelekea mchezo dhidi ya Simba tukiwa na wachezaji wetu wote"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’