Dube aishika pabaya Azam Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Apr 2024
Dube aishika pabaya Azam Fc

Jana Kamati ya TFF ya Sheria na Hadhi za wachezaji ilisikiliza shauri la mchezaji Prince Dube dhidi ya Azam Fc kuhusu mgogoro wa mkataba

Dube anapinga madai ya Azam Fc kumuongeza mkataba utakaodumu mpaka mwaka 2026 baada ya mkataba wake wa sasa unaotarajiwa kufika tamati mwezi Julai 2024

Za ndani ni kuwa imebainika ni kweli mkataba wa Dube na Azam Fc unamalizika mwezi Julai mwaka huu na huo mkataba mpya wanaodai Azam Fc haupo katika mfumo wa usajili wa TFF

Kwa mujibu wa kanuni, ili mkataba uwe halali lazima usajiliwe na kuthibitishwa na TFF kinyume na hivyo mkataba huo hautambuliki

Kamati imeahidi kutoa hukumu ya sakata hilo siku ya Jumamosi ambapo Mwanasheria wa Dube; Respicius Didas amesema ana imani kuwa mteja wake atatendewa haki na Kamati

Mwezi uliopita Azam Fc ilitangaza kumuweka sokoni Dube huku ikidai tayari imepokea ofa mbili kutoka klabu za Simba na Al Hilal ya Sudan

Hata hivyo Dube alisisitiza hataki kuuzwa, anachohitaji ni kuvunja mkataba wake uliobaki ili ajiunge na timu anayoitaka yeye

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’