Tulipambana ndani na nje ya uwanja - Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Apr 2024
Tulipambana ndani na nje ya uwanja - Gamondi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amewapongeza wachezaji wake kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo

Gamondi amedokeza kuwa haikuwa kazi rahisi kupata ushindi katika mchezo huo kwa kuzingatia uligubikwa na matukio mengi ya nje ya uwanja

"Kiwango cha daraja la juu kutoka kwa kundi hili la wachezaji na ujasili wa kupambana na mambo ya nje ya uwanja yaliyofanywa na wapinzani wetu wakati wa maandalizi kuelekea mchezo huu"

"Changamoto katika vyumba vya kubadilishia nguo, waamuzi, lakini katika mpira wa miguu kitu muhimu ni kucheza uwanjani na kwa hakika katika eneo hilo sisi ni bora"

"Hongera sana wachezaji, viongozi pamoja na Wananchi wote," aliandika Gamondi katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Jana Yanga ililazimika kutoingia katika vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kubainika kuna dawa imepuliziwa katika vyumba hivyo

Maafisa waliosimamia mchezo waliiruhusu Yanga kutotumia vyumba hivyo baada ya kujiridhisha uwepo wa harufu kali ya dawa tofauti na vyumba walivyotumia Simba

Mwamuzi wa kati Ahmed Arajiga alifanya kazi nzuri kwa sehemu kubwa ya mchezo huo lakini zipo nyakati maamuzi yake yalikuwa ya utata

Rafu nyingi zilionekana upande wa Yanga tu lakini pia ziliongezwa dakika 5 baada ya dakika 90 lakini mechi ilichezwa kwa dakika 8 zaidi

Katika dakika za majeruhi lipo tukio la Ibrahim Bacca kufanyiwa madhambi na Sadio Kanoute lakini akaamuru ipigwe kona kuelekea Yanga

Kabla ya mchezo zilienea tuhuma baadhi ya wachezaji kupigiwa simu kushawishiwa kwa fedha ili wacheze chini ya kiwango

Lakini jeshi la Wananchi lilikuwa imara kuhakikisha linaendeleza ubabe dhidi ya watani zao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’