Clement Mzize alifunga bao la ushindi kwa Yanga mara ya mwisho ilipokutana na Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa Novemba 08 katika uwanja wa CCM Mkwakwani
Leo tena Yanga itachuana na Coastal Union katika mchezo wa duru ya pili utakaopigwa uwanja wa Azam Complex, saa 12 jioni
Bila shaka Mzize atakuwa na nafasi ya kutumika katika mchezo huo ambao Yanga inazihitaji alama zote tatu
Katika msimu huu, Mzize amekuwa na mwendelezo mzuri akihusika katika mabao tisa yaliyofungwa na Yanga kwenye ligi kuu. Amepachika mabao manne na kutoa pasi tano za mabao
Stephane Aziz Ki ndio kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga akifunga mabao 15 na anaongoza mbio za kuwania ufungaji bora
Maxi Nzengeli amepachika mabao tisa wakati Mudathir Yahya akipachika mabao nane. Pacome Zouzoua ana mabao saba, Kennedy Musonda na Joseph Guede kila mmoja akiwa na mabao matatu