Gamondi aitaka nusu fainali kombe la FA

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Apr 2024
Gamondi aitaka nusu fainali kombe la FA

Kocha Mkuu Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Tabora United utakaopigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Azam Complex

Gamondi amesema anatambua mchezo huo utakuwa mgumu kwani ni mechi ya mtoano lakini jambo jema ni kuwa watakuwa katika uwanja wa nyumbani na wachezaji wameonyesha kuwa tayari kwa ajili ya mchezo huo

"Ni mchezo wa robo fainali, tunafahamu hatua kama hizi mechi zinakuwa ngumu. Tunajua ubora wa mpinzani wetu hivyo tunapaswa kujiandaa vyema kwa ajili ya dakika 90"

"Ninajivunia kuwa na timu yenye umoja mkubwa namna hii kuanzia ndani na nje ya uwanja, wachezaji wangu wana njaa na kiu ya mafanikio, nimefurahishwa sana na mazoezi ya hapo jana," alisema Gamondi

Aidha Gamondi amedokeza kuwa kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua anaweza kupata nafasi ya kucheza katika mchezo huo baada ya kuridhishwa na maendeleo yake

"Ameanza kufanya mazoezi ya timu, naweza kusema yuko tayari kurejea uwanjani, nitamungalia baada ya mazoezi ya mwisho leo"

"Katika mchezo wa kesho, ninaweza kumpatia dakika 20..30.. kulingana na utayari wake, " alisema Gamondi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’