Yanga imetinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB Bank baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United
Ulikuwa mchezo wa upande mmoja kwa muda mwingi Yanga ikitawala. Stephane Aziz Ki alihitaji dakika 35 tu kuiandikia Yanga bao la uongozi akipiga shuti kali nje kidogo ya 18 akipokea pasi kutoka kwa Kibwana Shomari
Kipindi cha pili Yanga iliendelea kutawala na kufanikiwa kuongeza mabao mawili kupitia kwa Kennedy Musonda na Joseph Guede
Baada ya kuwa nje ya uwanja wa wiki sita, Pacome Zouzoua leo amerejea akipata nafasi ya kucheza dakika 25 katika kipindi cha pili
Mpira wake mrefu ndio ulisababisha bao la tatu la Yanga lililofungwa Guede
Yanga imeungana na Ihefu Fc na Coastal Union ambazo zilitinga nusu fainali katika mechi zilizopigwa mapema