Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mabingwa watetezi Yanga watashuka uwanja wa Azam Complex kumenyana na Kagera Sugar katika mchezo utakaopigwa saa 1 usiku
Hii ni mechi muhimu kwa Yanga kwani alama tatu zitazidi kuwasogeza karibu na ubingwa wa tatu mfululizo
Licha ya kikosi chake kutopata muda wa kutosha wa maandalizi, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema wako tayari na dhamira yao ni kushinda mchezo huo
Kimahesabu Yanga inahitaji alama nane kutoka mechi tano zilizosalia lakini idadi hiyo inaweza kupungua kama Azam Fc na Simba zitadondosha alama katika mechi zao zilizobaki
Azam Fc na Simba zitachuana kesho katika mchezo ambao kama utamalizika kwa sare basi Yanga inaweza kwenda kutangaza ubingwa mkoani Morogoro katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar May 13
Gamondi amesisitiza kuwa kwa sasa hawafikirii ubingwa wanachofanya ni kuhakikisha wanashinda kila mechi inayokuja mbele yao hadi pale itakapothibitika kimahesabu hakuna timu itakayofikia alama zao