Waamuzi wamkera Gamondi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 May 2024
Waamuzi wamkera Gamondi

Jana Yanga ilijiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya NBC mapema baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex

Bao pekee la Yanga lilifungwa na Mudathir Yahya 'Mfalme wa Azam Complex' katika dakika ya 83

Lakini ulikuwa mchezo uliogubikwa na matukio mengi ikiwa ni pamoja na makosa ya waamuzi

Katika dakika ya 87 ya mchezo Yanga ilifunga bao kupitia kwa Joseph Guede lakini mwamuzi msaidizi namba 1 akakataa bao halali na kumnyima Guede bao lake la sita msimu huu

Ni tukio lililomkera Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ambaye baada ya mchezo nusura 'amuwambe makofi' mshika kibendera huyo

Gamondi alikerwa na kitendo cha mwamuzi huyo kukataa bao halali na kuinyima Yanga ushindi mnono

Kagera Sugar walicheza kwa kujilinda zaidi na kupoteza muda mwingi lakini pasi mpenyezo ya Aziz Ki katika dakika ya 83 ilitendewa haki na Mudathir aliyefunga bao lake la 9 msimu huu

Aziz Ki sasa amefikisha assist 8, akiongoza sawa na Kipre Junior wa Azam Fc. Ki pia anaongoza mbio za ufungaji bora akiwa na mabao 15 sawa na Feisal Salum wa Azam Fc

Ki ana mechi nne za kuhakikisha anabeba kiatu cha ufungaji bora msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’