Gamondi atahadharisha mechi za kuhitimisha msimu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 May 2024
Gamondi atahadharisha mechi za kuhitimisha msimu

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amewataka wachezaji wake kuongeza umakini na kutodharau mpinzani kwenye michezo iliyobakia kuhitimisha Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu

Gamondi amekiri kuwa kwa sasa kila mchezo ni mgumu kutokana na umuhimu wa pointi tatu kwa kila timu hivyo wanapaswa kuwa makini katika kila mchezo hasa ile watakayocheza ugenini

Yanga imebakisha michezo minne kumaliza ligi ambapo michezo miwili watacheza ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar na Dodoma Jiji na michezo miwili watacheza nyumbani dhidi ya Tabora United na Tanzania Prisons

Gamondi amesema michezo hiyo iliyobakia ni muhimu sana kwao lakini haitakuwa michezo rahisi kutokana na wapinzani wao kuhitaji pointi tatu ili kujinasua katika nafasi walizopo sasa kwenye msimamo

"Tunatakiwa kuongeza umakini zaidi, mchezo dhidi ya Kagera Sugar umetupa picha ya ugumu wa michezo ya mwishoni mwa ligi, kila timu inapambana kujinasua katika nafasi walizopo sasa hivi lazima wachezaji wangu wawe makini na kupambana muda wote wa mchezo ili kufikia malengo ya kutetea ubingwa wetu"

"Ni ngumu sana kupata pointi tatu kirahisi kwa timu zilizo kwenye eneo la hatari kwenye msimamo kwa sababu wanahitaji kujiondoa huko, kufanya hivyo wanapambana sana hasa wanapocheza na timu kubwa kama Yanga," alisema Gamondi

Jumatatu ya May 13 Yanga itakuwa mkoani Morogoro, uwanja wa Manungu kuikabili Mtibwa Sugar katika mchezo ambao kama Yanga itaibuka na ushindi inaweza kutangaza ubingwa mapema

Ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar utafanya Yanga ifikishe alama 71 ambazo ni Simba pekee inayoweza kuzifikia kama itashinda mechi zake zote zilizosalia

Pamoja na kuwa faida ya 'head-2-head' dhidi ya Simba, Wananchi pia wamefunga mabao mengi kuliko watani zao hao ambao watalazimika kushinda sio chini ya mabao manne katika kila mchezo ili wafikie idadi ya mabao ambayo Yanga wamefunga

Ni wazi Yanga itahitaji kumaliza kazi mkoani Morogoro ili wahamishie nguvu katika kombe la FA ambapo mchezo utakaofuata ni nusu fainali dhidi ya Ihefu Fc utakaopigwa May 19

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’