Juzi Msemaji wa Simba Ahmed Ali aliwashangaza wadau wa soka nchini baada ya kuweka bayana kuwa timu hiyo inamuunga mkono mchezaji wa Azam Fc Feisal Salum atwae tuzo ya ufungaji bora msimu huu
Feisal amefunga mabao 15 akiwa sawa na Stephane Aziz Ki wa Yanga lakini Ki akiwa na assist nane akiongoza sawa na Kipre Junior wa Azam Fc
Katika misimu miwili iliyopita, Yanga ilipigwa vita kali kuhakikisha haitoi mfungaji bora hasa baada ya kuwa imetwaa ubingwa
Hata msimu uliopita Saido Ntibazonkiza alipigiwa chapuo ya kushinda kiatu cha dhahabu akiwa amefunga mabao 17 sawa na Fiston Mayele licha ya kuwa Saido alifunga mabao mengi ya penati
Baada ya Aziz Ki kufungana mabao na Feisal, tayari tumeona kuna kanuni imetangazwa kuwa msimu huu kama wafungaji bora watakuwa wawili au zaidi, yule aliyefunga mabao machache ya penati ndio ataondoka na tuzo
Na ikitokea kigezo hicho kikashindwa kuamua, basi yule aliyecheza dakika chache zaidi atabeba tuzo
Katika mechi tatu zilizobaki Yanga haina cha kupoteza kwani tayari imetwaa ubingwa, kazi iliyobaki sasa ni kuhakikisha Aziz Ki anaibuka mfungaji bora
Aziz Ki amekuwa na mchango mkubwa katika ubingwa wa Yanga msimu huu, anastahili kushinda tuzo nje ya ubingwa huo