Hatukufahamu kama Lwandamina ameondoka - Nsajigwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Apr 2018
Hatukufahamu kama Lwandamina ameondoka - Nsajigwa
Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema hakuna aliyekuwa na taarifa juu ya kuondoka kwa kocha George Lwandamina na kwamba taarifa ya kuondoka kwake wameipokea kama 'suprise'.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana baada ya mchezo dhidi ya SIngida United uliomalizika kwa sare ya bao 1-1, Nsajigwa amesema kwa kiasi fulani tukio hilo limeathiri saikolojia ya wachezaji kuelekea mchezo huo.

"Hata kwenye familia mmoja wenu akipungua ambaye alikuwepo kwa mfano baba lazima kuna vitu havitakuwa sawa," alisema Nsajigwa.

Akizungumzia mchezo huo, Nsajigwa alisema Yanga ilihitaji kushinda, sare imekuwa ni matokeo tu lakini lengo kuu lilikuwa ni ushindi.

Amewapongeza wachezaji wa Yanga kwa juhudi zao za kusaka bao la ushindi hasa kwenye kipindi cha pili.

Nsajigwa amesema Singida United ni miongoni mwa timu bora msimu huu, ina kocha bora na wachezaji wenye hadhi sawa na wale walio kwenye vilabu Yanga, Simba na hata Azam FC.

Nae nahodha wa Yanga Nadir Haroub amesema sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaitta Dicha.

Nadir amesema wanafahamu wana kazi kubwa ya kutetea ubingwa baada ya mchezo huo wa marudiano. Hivyo watajipanga kuhakikisha wanapata ushindi April 29 watakapokutana na Simba.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’