Jana mlinzi wa kushoto wa Yanga Nickson Kibabage alishindwa kumaliza mchezo wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Ihefu fc baada ya kupata maumivu makali ya kichwa
Baada ya kupata huduma ya kwanza uwanjani, Kibabage alikimbizwa Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya matibabu zaidi
Klabu ya Yanga imeethibitisha kuwa hali yake imeimarika na pengine leo anaweza kuruhusiwa kurejea katika majukumu yake
Kwa mujibu wa Daktari wa Yanga, Moses Etutu, Kibabage alipata shida ya maumivu makali ya kichwa (Migraine)
Madaktari wamejiridhisha ilikuwa shida ya kawaida na sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu.
ADVERTISE HERE