Kiungo Jonas Mkude ni miongoni mwa wachezaji ambao wataendelea kuitumikia Yanga msimu ujao baada ya makubaliano ya mkataba mpya kufikiwa
Mkude alitua Yanga katika usajili wa msimu uliopita akipewa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuachana na Simba
Hakuanza vyema majukumu yake na Wananchi lakini baada ya kuuwasha moto katika mechi mbili za ligi ya mabingwa dhidi ya Mamelodi Sundown, Mkude akamshawishi Kocha Miguel Gamondi na hatimaye kujihakikishia nafasi ya kuendelea kuitumikia Yanga
Jana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji, Mkude 'aliupiga mwingi' akitawala dimba la kati sambamba na Zawadi Mauya ambaye nae 'anaskilizia' mkataba mpya
Mkakati wa Yanga ni kuhakikisha inawabakisha wachezaji wake bora pamoja na kuongeza nguvu katika maeneo ambayo yameonekana kuwa na mapungufu