Licha ya kuwa tayari ni mabingwa wa ligi kuu ambapo kesho watakabidhiwa ubingwa, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema malengo yake ni kuona wanashinda mechi mbili zilizosalia
Kesho Yanga itachuana na Tabora United katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni ambapo baada ya mchezo huo Yanga itakabidhiwa taji la ubingwa wa ligi kuu 2023/24
"Najua kesho tutakuwa na sherehe ya kukabidhiwa ubingwa baada ya mchezo dhidi ya Tabora United. Kabla ya sherehe hizo lazima tucheze mechi na mimi ni kocha ambaye sipendi kushindwa"
"Wachezaji wangu wanaweza kuwaambia mimi ni kocha wa aina gani, napenda tushinde kila mchezo. Moja ya malengo niliyoweka baada kushinda ubingwa, ni kushinda mechi tatu zinazofuata"
"Tutacheza kwa kuzingatia mbinu zetu na siku zote nawaambia wachezaji wangu lazima tufunge na tushinde kama timu. Tuposhinda mechi sifa ni kwa timu na sio mchezaji mmoja mmoja," alisema Gamondi
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, beki Ibrahim Bacca alisema fikra zao ni ushindi kwanza na sio sherehe za ubingwa. Baada ya mechi ndio watasheherekea