Aziz Ki bado hajamaliza kazi iliyomleta - Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 May 2024
Aziz Ki bado hajamaliza kazi iliyomleta - Hersi

Stephane Aziz Ki jana alifunga bao lake la 18 msimu huu na kuendeleea kuweka hai dhamira yake ya kuibuka mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC

Lilikuwa bao muhimu kwake hasa baada ya mshindani wake katika tuzo hiyo Feisal Salum kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 5-1 ambao Azam Fc waliupata dhidi ya Kagera Sugar

Aziz Ki alifunga bao la tatu la Yanga katika dakika za lala salama akifunga bao hilo kwa kichwa ikiwa mara yake ya kwanza kufunga bao kwa kichwa tangu alipotua Yanga misimu miwili iliyopita

Sasa habari njema kwa Wananchi ni kuwa huenda wakaendelea kumshuhudia Aziz Ki katika uzi wa Yanga msimu ujao

Baada ya tetesi nyingi kuhusu hatma ya kiungo huyo wa ushambuliaji, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said jana akatoa kauli yenye matumaini kwa Wananchi

Wakati akizungumza na mashabiki wa Yanga waliojitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa katika shamrashamra za ubingwa wa 30, Hersi alisema Aziz Ki ataondoka pale atakapokuma amemaliza kazi iliyomleta Tanzania

"Aziz Ki bado yupo sana kwani hajamaliza kazi iliyomleta Tanzania. Ataondoka nchini pale atakapomaliza kazi hiyo," alisema Hersi na kuibua shwangwe kwa mashabiki

Aziz Ki mwenyewe aliwahi kutoa kauli kama hiyo kuwa kilichomleta Yanga ni kushinda makombe lengo likiwa Ligi ya mabingwa na kazi hiyo bado hajaitimiza hivyo pale atakapoisaidia Yanga kucheza fainali na hata kubeba taji la ligi ya mabingwa basi ndio ataondoka

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’