Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inatarajiwa kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya kuwania kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Zambia
Kaimu Kocha Mkuu wa Stars Hemed Morocco jana alitangaza kikosi kitakachoingia kambni kwa ajili ya maandalizi hayo
Wachezji sita wa Yanga wamejumuishwa katika kikosi hicho ambacho kitaingia kambini baada ya ligi kuu ya NBC kuhitimishwa hapo kesho
Nyota wa Yanga walioitwa ni Aboutwalib Mshery, Bakari Nondo Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Nickson Kibabage, Mudathir Yahya na Clement Mzize
Watajiunga na kambi ya Stars baada ya mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Jumapili, Juni 02 visiwani Zanzibar
ADVERTISE HERE