Unaweza kusema msimu huu umekuwa bora sana kwa kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki
Takwimu zake zinazungumza kwa sauti kubwa zaidi na haishangazi kuona jina lake likitajwa kuwania tuzo mbalimbali
Huko Burkina Faso, Aziz Ki ameingia katika kinyan'ganyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka
Ki anachuana na Edmond Tapsoba wa Bayer Leverkusen na Issoufou Dayo wa RS Berkane
Pasipo na shaka, Aziz Ki anaweza kuondoka na tuzo moja au mbili za ligi kuu ya NBC akiwania tuzo ya mfungaji bora na MVP
ADVERTISE HERE