Gamondi kuwakabili Prisons kwa tahadhari

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 May 2024
Gamondi kuwakabili Prisons kwa tahadhari

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema amekiandaa kikosi chake kumaliza msimu vyema kwa kuibuka na ushindi katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa kesho Jumanne katika uwanja wa Azam Complex

Gamondi amesema kazi yake sio kubwa sana katika kiwanja cha mazoezi kwa sababu wachezaji wanafahamu nini wanapaswa kufanya uwanjani

Hata hivyo Gamondi amesema watakwenda kucheza mchezo huo kwa tahadhari kubwa kwani wana mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Azam Fc Jumapili, Juni 02

"Jana tulikuwa na mapumziko, leo tumerejea mazoezini kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mchezo huu wa mwisho msimu huu"

"Dhamira yetu haijabadilika, tunataka kumaliza msimu vyema lakini pia lazima tukumbuke tuna mchezo wa fainali Jumapili"

"Tumekuwa na muda wa kuwafuatilia wapinzani wetu kupitia mechi zao tano zilizopita hivyo tunafahamu vile tunakwenda kuwakabili"

"Kazi yangu sio kubwa sana katika nyakati hizi kwa sababu wachezaji wanafahamu mbinu na kile wanapaswa kufanya uwanjani," alisema Gamondi

Ni wazi kikosi cha Yanga kitakuwa na mabadiliko hapo kesho pengine baadhi ya wachezaji watapewa mapumziko kwa ajili ya mchezo dhidi ya Azam Fc

Mchezaji pekee ambaye ana uhakika wa kucheza mechi hiyo ni Stephane Aziz Ki anayewania tuzo ya ufungaji bora

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
1h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
4h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
9h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
13h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’